Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Equatorial Guinea wakomba bil 3.3

Equatorial Guinea(15).jpeg Mastaa Equatorial Guinea wakomba bil 3.3

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Obiang Nguema Mbatsogo jana alitangaza leo Jumanne, Januari 23 ni siku ya mapumziko nchini humo kusherehekea ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji wa fainali hizo za Afcon 2023, Ivory Coast.

Mbali na kutangaza siku hiyo kwa umma kusherehekea ushindi huo, Rais huyo ambaye aliutazama mchezo huo akiwa Ikulu ya Palacio de Malabo, pia aliizawadia timu hiyo bonasi ya Euro milioni 1 sawa na Sh2.7 bilioni kutokana na ushindi huo.

Wakati huo huo, Makamu wa rais wa nchi hiyo, Teodoro Nguema Obiang Mangue amenunua mabao hayo manne ya timu hiyo kwa Euro 20000 sawa na Sh546 milioni, Euro 50000 kwa kila moja.

Malengo ya timu hiyo katika fainali hizi ni kufika hatua ya nusu fainali kama ilivyokuwa mwaka 2015 ilipoandaa michuano hiyo, mwaka ambao Ivory Coast ilikuwa bingwa.

Guinea ya Ikweta imemaliza hatua ya makundi ikiwa kinara wa kundi lake A, baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare mmoja dhidi ya Nigeria.

Imemaliza ikiwa na pointi saba sawa na Nigeria zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku Ivory Coast ikimaliza ya tatu na pointi zao tatu na Guinea Bissau ikishika mkia bila pointi hata moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live