Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa England wapigishwa yoga kujiweka sawa

Wachezaji England Mastaa England wapigishwa yoga kujiweka sawa

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mastaa wa timu ya taifa ya England wamefanyishwa mazoezi ya yoga baada ya kocha wao Gareth Southgate kukiri wachezaji wake hawapo sawa kabisa.

Kocha huyo wa Three Lions, Southgate amewekwa kitimoto na sasa anapambana kuifanya timu yake kuwa tofauti kabla ya kufanyika kwa mchezo wao wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Slovenia, Jumanne.

Na Southgate alikiri kwamba wachezaji wake, akiwamo Harry Kane, walikuwa kwenye kiwango cha hovyo Alhamisi iliyopita kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Denmark.

Na kutokana na hilo, wachezaji hao walifanyishwa mazoezi ya yoga na mtaalamu Dr Rebekah Jade kwenye kambi ya timu hiyo huko Blankenhain.

Southgate alisema: “Hatukuwa tukikaba kabisa, hatukuonyesha kuitaka mechi kabisa.”

Kane alitolewa kwenye dakika ya 70 ya mchezo dhidi ya Denmark baada ya kushindwa kuonyesha makali, licha ya kwamba alifunga bao.

Southgate alisema: “Harry alicheza mechi moja tu kwa dakika 90 katika wiki tano au sita.”

Wakati akijiandaa na mechi ya mwisho dhidi ya Slovenia, Southgate alisema: “Tunajaribu kutazama kila kitu. Tunatazama kiwango chetu na mpinzani wetu ajayo, kuona tunafanya nini kwa ajili ya mchezo huo.”

Kwenye Kundi C, England inaongoza baada ya kukusanya pointi nne katika mechi mbili ilizocheza, ambapo imeshinda moja, dhidi ya Serbia na kutoka sare Denmark.

Inahitaji kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Slovenia, ambayo pia ina nafasi ya kuongoza kundi, endapo kama itashinda kwenye mechi hiyo, huku Denmark ikishindwa kuifunga Serbia katika mchezo mwingine wa mwisho kwenye kundi hilo.

Chanzo: Mwanaspoti