Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amepokea zawadi kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya klabu ya Al Nassr baada ya kufanikiwa kufunga mabao 40.
Ronaldo amefanikiwa kufunga mabao 40 mpaka sasa tangu mwaka umeanza Jambo lililofanya wachezaji wenzake ndani ya klabu hiyo kumzawadia keki iliyoandikwa mabao 40 ambayo ameyafunga akiwa na klabu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Ureno.
Staa huyo amefanikiwa kua mchezaji aliefunga mabao mengi kwa mwaka 2023 mpaka sasa akiwapika mastaa kama Earling Haaland na Kylian Mbappe ambao hawajafanikiwa kufunga mabao 40 mpaka sasa tangu mwaka uanze.
Gwiji huyo licha ya kua na umri wa miaka 38 lakini ameendelea kua alama kubwa katika soka, Kwani kulingana na umri wake haikua rahisi kufunga mabao 40 kwa mwaka na kushindana na vijana wadogo kama kina Mbappe na Haaland.
Cristiano Ronaldo mpaka sasa amekaa juu kabisa kwenye orodha ya wafungaji bora kwa mwaka 2023 akiwa na mabao yake 40, Huku akifuatiwa kwa karibu na Earling Haaland mwenye mabao 39 na Kylian Mbappe mwenye mabao 36 mpaka sasa.