Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa 5 Simba wampa mzuka Mgunda

Kanoute Sadio Ss Sadio Kanoute

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kurejea kikosini kwa mastaa watano wa Simba akiwamo Sadio Kanoute na Mohamed Ouatarra imempa mzuka kocha Juma Mgunda akisema chama limetimia na sasa anatumia muda wa wiki nzima kujiweka vyema kabla ya kuvaana na Singida Big Stars katika mechi ya Ligi Kuu Bara ugenini.

Mbali na wachezaji hao waliokuwa majeruhi, pia mabeki wa kulia Shomary Kapombe na Israel Mwenda pamoja na kiungo Victor Akpan na Mgunda alisema imemuongezea wigo wa kupanga kikosi kwenye mechi mbalimbali zilizopo mbele yao.

Mgunda alisema wiki moja aliyonayo kwa sasa kabla ya kuifuata Singida, wiki ijayo itatosha kuwaweka fiti wachezaji hao waliorejea baadhi yao wakicheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda mabao 5-0.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mgunda alisema wachezaji wake wamepata muda mzuri wa kujiandaa na ameweza kufanya nao mazoezi mepesi ili kuwapunguzia uchovu wa kucheza mechi nyingi mfululizo.

“Tumepata muda mzuri wa kujiandaa tuna mchezo Jumatano na Singida Big Stars utakuwa ni mchezo mgumu na wa ushindani, nafurahia, kuona wachezaji wangu waliokuwa majeruhi wamesharudi na wanaendelea na mazoezi,” alisema Mgunda na kuongeza;

‚“Sina kikosi maalum ambacho kimecheza mechi zaidi ya mbili mfululizo nimekuwa nikibadili mara kwa mara lengo langu ni kutoa nafasi kwa kila mchezaji hilo linanisaidia kupunguza presha ya wachezaji kucheza mara kwa mara kutokana na ratiba ilivyo.”

Mgunda alisema kurudi kwa Akpan na wenzake kunamuongezea nguvu ya kuamini kama ataweza kuendana na kasi ya ligi sambamba na ratiba kwa upande wao.

“Ukiwa na wachezaji wengi kikosini ambao wana hari nzuri ya ushindani wa namba kunaongeza chachu kwenye benchi la ufundi kuamua nani atumike leo na nani atumike mechi inayofuata lakini kukiwa na changamoto ya majeruhi mambo yanakuwa magumu.‚“

Wakati huohuo nyota wa kikosi hicho, Augustine Okrah alisema licha ya ugumu wa ratiba unaowakabili ila kwao ni nafasi nzuri ya kuonyesha ubora wao.

‚“Kila mchezo ni mgumu kwani tunacheza mechi moja kila baada ya siku tatu jambo ambalo sio rahisi, tutatapambana kadri ya uwezo wetu ili kuendeleza furaha kwa mashabiki zetu,” alisema.

Okrah aliongeza kitu kikubwa anachojivunia kwenye timu yao kwa sasa ni morali iliyopo baina yao wachezaji huku akiamini ushirikiano uliopo ndio silaha kubwa itakayowafanya kuchukua ubingwa walioukosa msimu uliopita. Simba imejipanga kubeba makombe yote msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti