Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa 12 watimia Simba, nani atoke aingie kipa?

Rfg Simba Ngoma Malone Mastaa 12 watimia Simba, nani atoke aingie kipa?

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukamilisha na kutangaza usajili wa kiungo mpya, Fabrice Ngoma, tayari kikosi cha Simba kimeenea kwa idadi ya wachezaji wa kigeni kuelekea msimu ujao 2023/24.

Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania, Klabu inatakiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12 kwa msimu husika wa mashindano, ambapo mapaka sasa idadi hiyo kwa Simba imetimia.

Endapo Simba watahitaji kusajili kipa wa kigeni kama tetesi zinavyodai kuchukua nafasi ya Aishi Manula ambaye ni mgonjwa, ama mchezaji yoyote anayecheza nafasi za ndani ya uwanja, wanahitaji kumwondoa mchezaji mmoja wa kigeni ili kuruhusu usajili huo ukamilike.

Wachezaji 12 wa kigeni wa Simba msimu ujao mpaka sasa ni hawa;

Clatouas Chota Chama - Zambia

Moses Phiri - Zambia

Peter Banda - Malawi

Pape Ousmane Sakho - Senegal

Sadio Kanoute - Mali

Aubin Kramo Kouamé - Cote d'Ivoire

Jean Toria Baleke Othos - Congo DR

Henock Inonga Baka - Congo DR

Fabrice Luamba Ngoma - Congo DR

Willy Essomba Onana - Cameroon

Saidi Ntibazonkiza - Burundi

Che Fondoh Malone Jr. - Cameroon.

Nani atoke ili aingine kipa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live