Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa 10 wanaoibeba Liverpool msimu huu

Skysports Premier League Liverpool 6340428 Mastaa 10 wanaoibeba Liverpool msimu huu

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Haya sasa... Liverpool iliyofufuka inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku ikifunga mabao mengi. Nani amekuwa mchezaji bora zaidi katika kikosi cha kocha Jurgen Klopp msimu huu ambaye amekuwa na mchango mkubwa?.

Mpaka sasa Liverpool imeendelea kufanya vizuri katika msimu wa 2023-2024, kulikuwa na mashaka kuhusu kiwango chao lakini imeonekana ina nguvu zaidi na imeleta ushindani katika mbio za kuwania ubingwa.

Aidha bado safu ya ulinzi imekuwa na mashaka zaidi hususan baada ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita.

Hata hivyo, ‘Liverpool Realoaded’ kama Jurgen Klopp anavyopenda kuwaita, imefungwa mechi mbili tu katika mashindano yote, hata mechi ya kwanza kati ya hizo ilipoteza kwa bahati mbaya, dhidi ya Tottenham ilipofungwa mabao 2-1 huku ikiwa pungufu.

Kwa mujibu wa GOAL.COM hawa hapa mastaa bora 10 wa Liverpool waliokiwasha msimu huu kulingana na asilimia walizoweka, pia wapo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya klabu ya mwaka 2023.

10. RYAN GRAVENBERCH (7.5/10)

Mholanzi huyo alikosa nafasi ya kucheza alipokuwa Bayern Munich, lakini sasa anafurahia soka akiwa Liverpool. Gravenberch tayari amehusika moja kwa moja katika mabao manne katika michuano yote, huku akifanya makubwa baada ya kuingia akitokea benchi dhidi ya Manchester City, Kiungo huyo (21) ana uwezo wa kumiliki mpira na ingawa sio mchezaji anayepangwa kikosi cha kwanza mara kwa mara lakini kila anapopata nafasi anaonyesha uwezo.

9. LUIS DIAZ (7.5/10)

Winga huyo alifunga bao dakika za mwisho dhidi ya Luton City na kuipa Liverpool pointi moja yenye thamani. Bao hilo alifunga wakati baba yake bado hajaokolewa na alipewa sifa kutokana na ukakamavu alioonyesha.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia ana uwezo wa kupiga chenga na kufunga.

8. DIOGO JOTA (7.5/10)

Mreno huyo anaweza kufunga mabao kila anapopata nafasi eneo la hatari. Licha ya kutoanza kikosi cha kwanza mara kwa mara, lakini mchango wake unakuwa mkubwa kila akitokea benchi.

Ni kati ya mshambuliaji hatari baada ya Mohamed Salah. Jota alikuwa na kiwango bora zaidi kabla ya kupata majeraha yaliyomweka nje ya dimba kwa muda mrefu, lakini sasa amekuwa fiti asilimia 100, kwani msimu huu amefunga mabao 10 katika mashindano yote aliyocheza.

7. DARWIN NUNEZ (8/10)

Mchezaji huyo wa Uruguay asiyetabirika ana mapungufu kwenye umaliziaji anapokuwa eneo la hatari. Lakini wakati mwingine anakuwa hatari anapokuwa eneo hilo. Baada ya kuanza mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu England, nyingine ameingia akitokea benchi, amejiweka kuwa chaguo la kwanza la mshambuliaji wa kati wa Klopp baada ya kufunga mabao saba na asisti tano.

Ushirikiano wake na Salah unaonekana kuwa na tija kwa Liverpool, kwani anaweza kuwa mtulivu mbele ya lengo.

6. ALEXIS MAC ALLISTER (8/10)

Safu ya kiungo ya ulinzi inaweza isiwe nafasi nzuri zaidi ya kwa Muargentina huyo lakini Mac Allister, ukweli ni kwamba anashika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji waliotengeneza mashambulizi mengi na wa tatu mwenye uwezo wa kumiliki mpira Liverpool.

Faida za kuwa na mchezaji mwenye kipaji cha ufundi anayefanya kazi vizuri jambo la kujivunia sana, pia amedhihirisha hilo wikiendi iliyopita dhidi ya Fulham.

5. ALISSON BECKER (8/10)

Amekuwa na mchango mkubwa kwa Liverpool msimu huu, licha ya kuizawadia bao Man City katika sare ya bao 1-1 kipa hiyo amepata majeraha na anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa wiki kadhaa.

Kwa heshima zote, Klopp atakuwa anamuombea arejee uwanjani haraka kwani ndio anayetegemewa.

Alicheza mechi tatu za ligi kabla ya kuumia na alionekana kuwa kiungo muhimu kwa Liverpool.

Matokeo bora zaidi ya msimu huu, ni ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle huku Liverpool ikiwa pungufu.

4. DOMNIK SZOBOSZLAI (8.5/10)

Kiungo huyo wa kimatataifa wa Hungary, alijiunga na Liverpool akitokea RB Leipzig kwa Pauni 60 milioni, usajili uliopita. tangu alipotua ameonyesha kiwango bora na mhimili wa Liverpool dimba la kati.

Szoboszlai ndo mchezaji anayeongoza kumiliki mpira zaidi Liverpool, amepiga pasi 809 zilizokamika eneo sahihi, huku Salah akiwa mchezaji pekee alitengeneza nafasi za kufunga zaidi ya viungo.

3. VIRGIL VAN DIJK (8.5/10)

Baada ya kuanza vibaya msimu huu kufuatia kadi nyekundu aliyolimwa kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle Agosti mwaka huu, beki huyo mwenye umri wa miaka 32 mchango wake umeanza kuonekana.

Kwa mtazamo wa Klopp hakuna mchezaji anayemvutia zaidi kama Van Dijk kwani amefanya mambo makubwa, kupiga pasi zenye faida, na kukaba. Safu ya ulinzi wa Liverpool inatetereka endapo Mholanzi huyo akikosekana.

2. TRENT ALEXANDER-ARNOLD (8.5/10)

Beki huyo alipondwa sana kutokana na kiwango chake, hata hivyo amedhihirisha kuwa ana kipaji cha kucheza soka. Klopp anapenda kumpa Alexander-Arnold uhuru wa kucheza- ndo maana wakati mwingine anampanga kama kiungo wa kati badala ya beki.

Beki huyo ameshangaza mashabiki dhidi ya Man City na Fulham akicheza kama kiungo, na alikuwa shujaa katika ushindi wa mabao 4-3 wikiendi iliyopita.

Alexander-Arnold alipata majeraha mwanzo wa msimu lakini amefanikiwa kufikia kiwango kikubwa zaidi mwezi mmoja uliopita, na kukabidhiwa kitambaa cha unahodha kama msaidizi wa Van Dijk.

1. MOHAMED SALAH (9/10)

Ni sawa na kusema Liverpool ilifanya jambo sahihi kukataa ofa ya Pauni 150 milioni kutoka Saudi Arabia.

Salah amekuwa wa kuvutia msimu huu, akitoa aina ya uchezaji madhubuti ambao unaweza kuendeleza changamoto ya ubingwa.

Tayari amefikisha mabao 13, hata kama timu ikitoka sare, fowadi huyo wa kimataifa wa Misri atapambana kuisaidia timu hadi dakika ya 90.

Salah sio tu anaongoza katika orodha ya mchezaji bora wa msimu Liverpool, anaweza pia kushinda kiati cha dhahabu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu England akichuana vikali na Erling Haaland wa Man City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live