Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Massimiliano Allegri aweka ngumu kwa Morata

Allegri Morata Morata akiwa na Allegri

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri amemaliza mzizi wa fitna juu ya tetesi za uhamisho wa Alvaro Morata kujiunga na Barcelona.

Morata amekuwa akihusishwa sana na Barcelona hivi karibuni, kukiwa na mapendekezo kwamba anaweza kumaliza mkataba wake wa mkopo wa miaka miwili mapema zaidi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alidaiwa kujiunga na Barcelona kwa mkopo kwa miezi sita, kukiwa na nia ya kufanya uhamisho wa kudumu.

Lakini inaonekana kwamba dili hilo halitafanyika tena, baada ya mkufunzi wa Juventus Allegri kuzungumzia uhamisho huo.

Allegri alikutana na Morata mapema wiki hii, na ameweka wazi bila shaka kwamba dili hilo halitafanyika.

Alinukuliwa na Soka Italia akisema: “Nilimwambia Alvaro kwamba anabaki hapa, haondoki Juventus, mwisho wa hadithi.”

Hilo linaweza kuwa pigo kubwa kwa Barcelona, ambao walikuwa na matumaini ya kuimarisha safu yao ya mbele msimu huu wa joto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live