Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Massimiliano Allegri agoma kung'atuka Juventus

Allegri Massimiliano March Massimiliano Allegri

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri na mkurugenzi wa michezo Federico Cherubini watalazimika kusalia klabuni hapo baada ya awali kuwa na nia ya kujiuzulu kufuatia bodi nzima ya wakurugenzi kujiuzulu nyadhifa zao Jumatatu usiku.

Kuondoka kwa Rais Andrea Agnelli na mwenzake kumeacha hali ya wasiwasi mjini Turin, huku wachezaji wakiwa na wasiwasi kuhusu kitakachofuata.

Kulingana na Jarida la “La Gazzetta dello Sport”, Allegri na Cherubini wote walikuwa tayari kuondoka kwa sababu ya uaminifu wao kwa Agnelli, ambaye alishinda mataji tisa mfululizo ya ligi kati ya 2011-12 na 2019-20 wakati wa utawala wake, lakini walizungumziwa na klabu hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oxor John Elkann, nae atasalia kwa sasa.

Huku klabu ikiwa na msukosuko, kuondoka kwa Allegri na Cherubini kungekuwa pigo lingine ambalo lingeweza kuhatarisha mustakabali wa kimichezo wa Juventus.

Lakini sasa wamechagua kubaki katika majukumu yao, na Allegri tayari amechukua hatua kujaribu kuwatuliza wachezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live