Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Massanza: Yanga inatuonesha Fainali ya CAFCL inawezekana

Simba Yanga WA0007 Massanza: Yanga inatuonesha Fainali ya CAFCL inawezekana

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Massanza amesema licha ya Simba SC kufika robo fainali ya michuano ya CAF mara nyingi zaidi kwa timu za Tanzania, lakini yanga inaonesha kuwa upo uwezekano wa kufika mpaka fainali ya michuano hiyo.

Massanza amesema hayo baada ya Simba na Yanga kufanikiwa kutusua hatua ya robo fainali ya CAFCL huku Yanga ikiwa na rekodi ya kuingia fainali ya CAFCC msimu uliopita dhidi ya USM Alger licha ya kupoteza ubingwa huo kwa kanuni ya bao la ugenini.

Yanga ilitinga robo fainali ya CAFCL mnamo Februari 24, 2024 kwa kuitungua CR Belouizdad, Mabingwa wa Algeria mara 4 mfululizo kwa bao 4-0 katika Dimba la Mkapa.

"Kijana kacharuka, kaweka rekodi sawa leo, unaweza usifurahie sana lakini ukweli ni ukweli. Ni kweli Simba imechora ramani ya soka letu kushindana kimataifa. Kwa sasa hakuna timu kwenye ukanda huu Afrika inatamani kukutana na timu kutoka Tanzania. Achilia mbali Simba.

"Kwa mfano, Singida tu tulimkanda Future pale Azam Complex kwa kiburi ambacho Simba walikianzisha, ukweli ni ukweli, lakini Yanga imeonesha nia ya kuset standard ya juu zaidi.

"Yanga inaona robo fainali haitoshi kwahiyo inatuonesha kufika Fainali inawezekana. Imeanzia kule Shirikisho na bila shaka itaweka rekodi mpya Klabu Bingwa.

"Ni kawaida, hata walimu waliotufundisha huko nyuma wengi wao tumewaacha mbali sana kimaisha na kitaaluma. Huu sasa ndio ushindani unaotakiwa. Tuendelee kutambiana records hivi hivi kulisukuma soka letu," amesema Massanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live