Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Massanza: Wanaosema Singida tumeyumba hawajielewi

Massanza Jr Msemaji wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ameandika msemaji wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza

"Nilichogundua timu zetu zinahitaji zaidi wachezaji matured wanaoweza kuipambania timu na sio kuipambania mikataba yao peke yake.

Ukiwa na wachezaji wa mishahara na mikataba, mtakuwa mnahangaika na vipengele vya sheria kila siku badala ya kuhangaika kupata matokeo uwanjani.

Nafurahia uelekeo wa timu yetu kwa sasa, hatupati matokeo mazuri katika kipindi hiki cha mpito, lakini tunaona maturity ya wachezaji wetu na dhamira ya kupambana kutafuta matokeo.

Wenye maono mafupi watadhani tumeyumba, wenye maono ya mbali watajua tunachokilenga.

Muda utasema!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live