Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud aachiwa faili la Mkandala

Mkandala Pic Data Masoud aachiwa faili la Mkandala

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha mpya wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma amepewa faili la kiungo nyota wa timu hiyo, Cleophas Mkandala na kuachiwa kuamua hatma yake wakati mkataba wake ukimalizika mwisho wa msimu.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, ambayo jana usiku ilikuwa ikiumana na Mbeya Kwanza, Fortunatus Johnson alisema wameanza mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo huyo, ila kocha Masoud ndiye atakayetoa majibu ya mwisho kama atasalia au la.

“Kwa muda ambao kocha amekaa tayari amefahamiana vizuri na wachezaji wake nasi kama viongozi jukumu letu kubwa ni kumtimizia mahitaji yake, hivyo nani atabaki au kuondoka hilo lipo juu yake,” alisema.

Aliongeza licha ya kocha naye kupewa mkataba hadi mwisho mwa msimu ila kuna kipengele cha kumwongezea zaidi ndio maana wao kama viongozi wamempa nafasi hiyo kubwa ya uamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya timu yao.

Kocha huyo msaidizi wa zamani wa Simba alitambulishwa rasmi katika timu hiyo Februari 24, mwaka huu baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Mbwana Makata kutimuliwa kufuatia matokeo mabaya mfululizo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz