Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud Djumaa atimuliwa Dodoma Jiji

Masoud Djuma 1080x640 1 Masoud Djumaa

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa timu ya  Dodoma Jiji umevunja benchi la ufundi la klabu hiyo lilokuwa likiongozwa na Masoud Djumaa kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya klabu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Wengine waliotupiwa  virago ni pamoja na kocha msaidizi Mohammed Muya,Kocha wa makipa Adam Meja ambaye inadaiwa amejiunga na Simba Queens.

Dodoma Jiji mpaka sasa imecheza michezo sita ikishinda mmoja na kutoa sare miwili huku ikipoteza mitatu katika msimamo inashika nafasi ya 14.

Djuma amedumu katika klabu hiyo kwa miezi nane  ambapo uongozi wa klabu hiyo ulimtambulisha Februari mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo oktoba 10 mwaka huu na uongozi wa klabu hiyo ilieleza kuwa menejimenti ya klabu hiyo imefikia maamuzi hayo ili kupata wasaa wa kuliunda upya benchi hilo.

“Uongozi wa klabu unawashukuru kocha mkuu pamoja na benchi lote la ufundi kwa mchango wao mkubwa ndani ya klabu yetu na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya,”ilieleza taarifa hiyo.

Pia ilieleza kwa sasa klabu hiyo  itakuwa chini ya usimamizi wa kocha wa timu ya vijana Omary Mohammed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live