Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud Djuma kuchukua Mikoba ya Makata

Masoud Pic Masoud Djuma Irambona

Wed, 23 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ni Rasmi sasa, aliyewahi kuwa Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma Irambona, ndiye Kocha mkuu mpya wa Dodoma Jiji.

Licha ya kwamba, Djuma bado hajawasili mjini Dodoma, ila taarifa za uhakika zimethibitisha wazi kwamba, akiwasili tu Dodoma atatambulishwa kuwa Kocha mpya baada ya kukubaliana kila kitu akiwa kwao nchini Burundi.

Djuma, anatarajiwa kutangazwa rasmi kesho Alhamisi, Saa sita mchana baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, akianza na kazi ya kuibadilisha timu hiyo kwa msimu uliobaki.

Kocha huyo atasaini mkataba wa miezi sita, ikiwa ni lengo la kuibakisha timu hiyo Ligi Kuu, ndipo mkataba utakapoongezwa baada ya kufikia lengo hilo.

Bosi wa kamati ya usajili wa wachezaji na makocha wa timu hiyo, Fredrick Mwakisambwe amesema kila kitu kinakwenda kama walivyopanga na wakitarajiwa kukamilisha dili hilo kesho Alhamisi kabla ya kocha huyo kuanza rasmi kuinoa timu hiyo, akianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

"Kila kitu kuhusu kinaenda vema kama tulivyopangilia, tunaamini kesho ndipo tutatangaza rasmi na kumtambulisha Kocha huyo, ili aanze kazi kuelekea mchezo wetu wa ugenini dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting" alisema Mwakisambwe.

Katika hatua nyingine, taarifa ya kuachana na Makata kama Kocha mkuu, imeacha wazi hatma ya msaidizi wake Renatus Shija kama ataendelea kuwa msaidizi ama vinginevyo.

Mwanaspoti linaweza kuthibitisha kwamba, Kocha huyo msaidizi pia naye hataendelea kuwa kwenye timu hiyo, nafasi yake ikitarajiwa kuzibwa na aliyekuwa Kocha wa Fountain Gate FC na Fountain Gate Princess kabla ya kujiuzulu wiki iliyopita, Mohammed Muya.

Muya aliwahi kuhudumu kwenye nafasi hiyo ya Kocha msaidizi, akiwa na Jamhuri Kiwhelo 'Julio' wakati timu hiyo ikiwa daraja la kwanza (sasa Championship).

Makocha wote wawili wanatarajiwa kutangazwa kesho Alhamisi mkatika ofisi za Halmashauri ya Jiji.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz