Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoud Djuma arejesha tumani Dodoma Jiji

Dodoma 2 Djuma Masoud Djuma arejesha tumani Dodoma Jiji

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Dodoma Jiji, umeibuka na kusema una imani timu hiyo itafanya vizuri na kufanikisha malengo yake ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Masoud Djuma.

Februari 24, mwaka huu, kocha huyo raia wa Burundi ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, alitambulishwa rasmi kikosini hapo akichukua mikoba ya Mbwana Makata.

Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fourtnatus Johnson, alisema: “Tuna imani na Kocha Masoud Juma, mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting ambao tulifanikiwa kupata pointi moja ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na sisi japokuwa hakukaa kwenye benchi la ufundi kwa sababu bado hatujamaliza mchakato wa vibali vyake, lakini tutegemee kumuona hivi karibuni.

“Tunatarajia kuweka kambi nje ya Dodoma kuelekea maandalizi yetu dhidi ya Azam Machi 4, dhumuni kuu la kuweka kambi hiyo ni kwa ajili ya kumpa kocha nafasi ya kukaa na wachezaji wake na kufanya tathmini ambayo itamsaidia kuweka mipango ya ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live