Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mason Greenwood kutua Lazio

Greenwoodz Mason Greenwood kutua Lazio

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lazio imeonesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood.

Timu hiyo ya Italia imepanga kukiimarisha kikosi hicho kinachonolewa na Marco Baroni. Ripoti za nchini Italia zinasema kuwa timu hiyo inataka wachezaji makinda wawili, mmoja wao ni Greenwood.

Nyota mwingine ni Lazar Samardzic kutoka Udinese ni miongoni mwa nyota wanaotakiwa na Lazio.

Kwa mujibu wa Gianluca Di Marzio, Lazio ilituma wajumbe kwenda Manchester kujadili uwezekano wa kumnunua Greenwood.

Di Marzio anaongeza kuwa Lazio wamemfuata Greenwood kwa muda, baada ya kuhusishwa na uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji huyo mwaka jana kabla ya kusaini mkataba wa muda na klabu ya La Liga, Granada.

Greenwood pia amekuwa akihusishwa na kuhamia Juventus, Napoli na Valencia. Inafahamika kuwa anapendelea kubaki Uhispania kwa vile hana mustakabali wa kuendelea Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live