Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mason Greenwood akimbilia China, Ten Hag atoa tamko

Mason Greenwood Mason Greenwood akimbilia China, Ten Hag atoa tamko

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mason Greenwood Inaripotiwa kuwa yuko tayari kufufua maisha yake ya soka nchini China iwapo Manchester United itavunja mkataba wake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa yuko chini ya uchunguzi wa ndani wa klabu iwapo ataingia tena kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag.

Hali hii inakuja baada ya mashtaka ya madai ya ubakaji na shambulio dhidi ya Greenwood kutupiliwa mbali na waendesha mashtaka wiki hii.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Greenwood amekubali kwa huzuni mchakato wa ndani wa United ambao unatoa muda wa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.

Jarida hilo linadai kwamba Greenwood alipofungiwa awali na United mwaka jana, muda mfupi baada ya kukamatwa Januari, aliapa kutoichezea klabu hiyo tena.

Chanzo kimoja kilisema: “Wakati huo alikuwa akisisitiza kwamba hataki kuvaa jezi nyekundu tena, Alihisi kama klabu haikuwa upande wake.

“Alisema atafurahi kwenda kucheza China mradi tu analipwa vizuri na anacheza.”

“Mtazamo wake unaweza kuwa kweli katika miezi michache iliyopita, lakini hakuwa na furaha hata kidogo.”

Wengine waliliambia gazeti la The Sun kuwa wanahofia Greenwood angekabiliana na wimbi la unyanyasaji ambao bila shaka angekabiliana nalo kutoka kwa mashabiki wapinzani iwapo atarejea kwenye EPL.

Greenwood Amesalia kwenye orodha ya kikosi cha United cha EPL, baada ya kutajwa miongoni mwa wachezaji wao wa chini ya miaka 21 mwanzoni mwa msimu. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa na zawadi ya ukaribisho ukijiunga. Bashiri hapa.

Hata hivyo hakukuwa na dalili ya jina la Greenwood kwenye orodha ya kikosi United iliyosajiliwa na UEFA kwenye raundi ya mtoano ya Europa, ambayo ilitajwa Ijumaa.

Meneja wa United Ten Hag alikataa kuzungumzia zaidi hali ya Greenwood alipofanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Jumamosi ya ligi dhidi ya Crystal Palace.

Ligi kuu ya China ilivutia wanasoka wengine mwaka wa 2017 wakati mastaa kama Carlos Tevez, Oscar na Alexandre Pato walihamia huko kwa sababu ya mishahara mikubwa iliyotolewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live