Winga wa Manchester United Mason Greenwood kijana wa England mwenye umri wa miaka 21 ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili ya kutuhumiwa kumbaka na matumizi ya nguvu dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake.
Greenwood alikamatwa Januari 2022 ambapo tangia kipindi hicho hajawai kucheza mchezo wowote mpaka wakati huu ambapo kesi yake imefutwa.
Baada ya kuwa huru, Greenwood ameandika kuwa kufuatia kuwa huru ni sawa na kufufuka upya ambapo amewashukuru marafiki na familia kwa kuwa naye kwenye kipindi chote cha mpito.
Mahakama ambayo ilikuwa inahusika na kesi hiyo imesema sababu ya Greenwood kubaki huru ni baada ya mlalamikaji/shahidi kuondoa ushiriki wake kwenye kutoa ushahidi.