Paul Pogba amelaumu changamoto alizopata tangu alipotua Juventus akidai zilisababishwa na matatizo ya kisaikolojia, vilevile alisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Mfaransa huyo alirejea Juventus katika dirisha la usajili la kiangazi lililopita baada ya mkataba wake kumalizika Manchester United, Hata hivyo, mambo yalibadilika kwani Pogba alisumbuliwa na jeraha la kwanza wakati wa maandalizi ya msimu mpya na licha ya kushauriwa kufanyiwa upasuaji, aligoma lakini hakufanikiwa kupona haraka.
Baadaye alilazimika kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi Septemba mwaka jana, na akakosa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka jana.
“Majeraha yangu yalitokana na matatizo ya kiakili. Msimu uliopita ulikuwa mgumu sana kwangu, naamini nitashinda vikwazo hivi na nitarejea dimbani,” alisema Pogba.