Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa yatimua uongozi kuinusuru isishuke Daraja

Mashujaa Kukwepa Kichapo Cha Sita Leo Dhidi Ya Tabora United Mashujaa yatimua uongozi kuinusuru isishuke Daraja

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya mpira wa miguu Mashujaa ya mkoani Kigoma imetangaza utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuinusuru timu hiyo kushuka daraja ikiwemo kuuondoa uongozi uliokabidhiwa timu baada ya timu kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara na kuurejesha uongozi uliohangaika na timu hiyo kuipandisha daraja.

Mwenyekiti wa timu ya Mashujaa, Meja Abdul Tika ambaye amerudishwa tena kuiongoza timu hiyo ametangaza hayo kwenye mkutano wa pamoja uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma, baina ya uongozi wa timu ukiongozwa na Meja Tika, Kamati ya Hamasa ya Mkoa ikiongoza na Omari Singso na wapenzi wa soka wa mkoa huo.

Mkutano huo unafuatia matokeo mabaya ya timu hiyo ya Mashujaa ambayo imepoteza michezo saba mfululizo huku kukiwa na sintofahamu baina ya uongozi wa timu na mashabiki wa timu hiyo kwa kile kilichoonekana uongozi wa Jeshi kutotaka kuingiliwa kwenye majukumu ya kusimamia timu.

Wakizungumza kwenye mkutano huo wapenzi wa soka mkoani Kigoma wamesema kuwa wameshangazwa kuona uongozi wa Jeshi unaondoa viongozi waliopandisha timu, kuondoa idadi kubwa ya wachezaji na kutoshirikisha wananchi kwenye mipango mbalimbali ya kutafutia timu ushindi.

Mmoja wa wapenzi waliohudhuria mkutano huo, Salehe Nassoro amesema kuwa baada ya timu kupanda ligi kuu uongozi wa jeshi ulishindwa kufanya usajili wa maana na hivyo kuleta wachezaji wa kiwango cha chini ambao wameshindwa kuonyesha uwezo wao na kuifanya timu kufika hapo ilipo.

Naye, Hanzuruni Kibera alisema kuwa licha ya wachezaji kuwa na viwango vidogo vya kuweza kushindana wengi hawakuwa na nidhamu na walikuwa wakionekana kwenye mabaa wakizurula hovyo hadi siku ya mechi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live