Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa yaipiga Simba kwenye mshono, yaifurusha kombe la CRDB

Simba Out Mashujaa yaipiga Simba kwenye mshono, yaifurusha kombe la CRDB

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wameondoshwa rasmi na Mashujaa FC katika mashindano ya CRDB Confederation kwa kufungwa penalti 6-5.

Simba wamefurushwa kwa mikwaju hiyo ya penalti baada ya dakika tisini kumalizika kwa sare ya 1-1 katika dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya 5 ya mchezo kupitia kwa Reuliant Lusajo ambalo lilidumu mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili, Simba waliingia kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha goli dakika ya 51 kupitia kwa 'super sub' Fredy Michael aliyeingia kuchukua nafasi ya Par Omary Jobe.

Kipigo hiki ni maumivu baada ya maumivu kwani Simba wametoka kufurushwa na Al Ahly kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live