Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa yaikandamiza bao 3 KMC Uwanja wa Lake Tanganyika

Mashujaa Vs KMC Mashujaa yaikandamiza bao 3 KMC Uwanja wa Lake Tanganyika

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Jeremanus Josephat dakika ya 12, Hassan Cheda dakika ya 22 na Relliants Lusajo dakika ya 60.

Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati KMC inabaki na pointi zake 33 za mechi 26 pia nafasi ya tano katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.

Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live