Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa wataweza kushikilia bomba?

Mashujaa Vs Kagera.jpeg Mashujaa wataweza kushikilia bomba?

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wanetu Mashujaa FC wameanza kibabe Ligi Kuu ya NBC msimu huu ambapo katika mechi zao tatu za mwanzo hawajapoteza hata moja wakishinda mbili na kutoka sare moja.

Walianza kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 kisha wakatoka sare tasa na Geita Gold na baada ya hapo wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu SC.

Ushindi huo umeonekana kukonga nyoyo za mashabiki wengi wa timu hiyo na baadhi yao wameanza kuwa na imani kwamba watamaliza wakiwa ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kwa namna ambavyo timu yao imecheza kwenye mechi tatu za mwanzo, wana haki buana ya kutamba maana wachezaji wamekuwa wakijituma na kufanyia kazi vyema maelekezo wanayopewa na benchi lao la ufundi.

Hata hivyo, hizo mechi tatu za mwanzo zote wamechezea nyumbani hivyo wamepata faida ya kuuzoea uwanja lakini pia kuwa na hamasa ya mashabiki wao ambao wamekuwa wakiisapoti vilivyo timu yao.

Wana michezo 27 imebaki mbele yao ambayo wanatakiwa kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri ili kututhibitishia kwamba hicho walichoanza nacho sio nguvu ya soda.

Baada ya kuanza vizuri, wanapaswa kukumbuka kwamba kazi iliyopo mbele yao ni nzito zaidi ya ile waliyoifanya dhidi ya Geita Gold, Kagera Sugar na Ihefu kwani watakuwa na michezo mingi ugenini na baadhi ya migumu nyumbani.

Chanzo: Mwanaspoti