Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa wanaitaka Ligi Kuu

Mashujaa Pic Mashujaa wanaitaka Ligi Kuu

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuambulia sare ya mabao 2-2 mwishoni mwa wiki ikiwa ugenini dhidi ya Kitayosce, hivi sasa Mashujaa imeanza kujihakikishia kupata nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Mashujaa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 35 sawa na Pamba nafasi ambazo zitawawezesha kucheza hatua ya mtoano dhidi yao na mshindi kucheza na timu kutoka Ligi Kuu.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa timu ya Pamba kucheza hatua ya mtoano kwani msimu wa 2020/21 iliondolewa na Coastal Union katika hatua ya mwisho ikiwania kupanda Ligi Kuu.

Mashujaa ambayo haijawahi kucheza Ligi Kuu wala hatua ya mtoano kama itamaliza nafasi hiyo itakuwa mafanikio makubwa kwao kwenye Ligi ya Championship.

Kocha wa Mashujaa, Rashidi Iddi ‘Chama’ alisema wanachoangalia ni kupata alama tatu katika michezo iliyosalia.

“Unajua ili ufanikiwe kwenye mipango yako lazima uhakikishe haupotezi michezo yako ambayo itazidi kukuweka kwenye nafasi nzuri zaidi. Tulikuwa na ratiba ngumu mbele ya Kitayosce lakini tukafanikiwa kuondoka na alama moja ambayo kwetu muhimu sana kuliko kukosa kabisa alama,” alisema Chama.

Aliongeza ushirikiano wanaoupata kutoka kwa uongozi ndio chachu ya kuzidi kupambana na hata wachezaji wamekuwa kwenye morali kubwa.

Baada ya kumalizana na Kitayosce juzi timu hiyo ililala Dodoma ikiwa inaelekea Songea kukabiliana na Mbeya Kwanza katika mchezo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Majimaji.

Chanzo: Mwanaspoti