Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa vs Azam nani anapasuka leo?

Azam Vs Mashujaa Leo Mashujaa vs Azam nani anapasuka leo?

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC itakuwa na kibarua kigumu wakati itakapokuwa inacheza na Mashujaa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma huku timu zote zikiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo yao miwili mfululizo.

Mechi ya mapema saa 8:00 itazikutanisha Singida Big Stars itayokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Liti, mjini Singida.

Timu zote zinakutana zikitoka kupoteza michezo yao ya mwisho na Singida ilichapwa mabao 2-0 na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga kwenye Uwanja wa Benja-min Mkapa, jijini Dar es Salaam sawa na Ihefu pia iliyochapwa na Simba 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live