Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa kuna ni ni huko?

Ty Mashujaa Mashujaa kuna ni ni huko?

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mashujaa ni miongoni mwa timu ngeni ndani ya ligi kuu Tanzania bara ambazo zilipanda daraja Kuja ligi kuu NBC , Ilianza msimu kwa kuonyesha Ubora mkubwa sana ambao watu wengi walianza kuamini kuwa imekuja kutoa changamoto kwa vilabu vikongwe vya NBC,

kwani kwenye michezo yao minne ya mwanzo NBC walicheza bila kupoteza , bila kuruhusu hata goli moja.

Baada ya kuendelea na ushindi , tuliiandika na kuisifia sana juu ya wanachokifanya kwani team iliyopanda ligi kuu kucheza michezo minne bila kuruhusu Goli si jambo dogo,

TAKWIMU ZIMEANZA KUWAKATAA SASA: Lakini Hadi kufika muda huu , Mechi zote zilizofuatia wamepoteza, michezo 4 mfululizo wameruhusu magoli 9 na wamefunga goli 1 tu na sasa wapo nafasi ya 2 kutoka mkiani

WALIOPANDA: Niliwahi kuandika kuwa , Ubora wa timu zinazopanda ligi kuu ndiyo huwa unaakisi ubora wa ligi yeyote Ulimwenguni , Kama timu inayopanda ligi kuu itashindwa kuzipa changamoto hizi timu ambazo zipo ligi kuu kitambo tena kwa daraja la kati,

Ni vigumu kuamini mashujaa na wengine waliopanda ligi kuu kuwa wamekuja kuzi chalenji Yanga, Simba na Azam, Simaanishi kuwa hawana usajili bora No ila namaanisha muendelezo wa matokeo bora muda mrefu ndio shida ,

Sijajua ni nini ila nahisi kuna kitu wanapitia , Yawezekana aina ya usajili waliofanya ulikuja kwa nguvu kubwa sana ili kuuaminisha uongozi na ili hali haupo hivyo ama Wapinzani wameijua njia wanayopitia ndio maana imekuwa kawaida kwa wao kupoteza kwa maana mfumo wa Mwalimu ama hata type ya uchezaji wa wachezaji walio nao,

Ligi inaendelea kuwa ngumu kadri siku zinavyosonga na vilabu vinazidi kuongeza wachezaji wenye ubora bila kujali mabenchi ya ufundi yanazidi kuboreshwa day to day,

KWA VILABU VYOTE: Ikiwa mzunguko wa kwanza ulishindwa kubaini madhaifu yako vya kutosha basi jiandae na dhahama ya magoli kwa mzunguko wa pili

Mashujaa Mnakosea wapinama tuonane dirisha dogo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: