Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa amewahi kuitoa Simba hatua kama ya leo

Mashujaa Amewahi Kuitoa Simba Hatua Kama Ya Leo Mashujaa amewahi kuitoa Simba hatua kama ya leo

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashujaa FC V/s SIMBA ni mechi ya CRDB Bank Federation Cup hatua ya 16 Bora, mechi itachezwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kuanzia saa 10:00 jioni.

Msimu huu ni mara ya pili timu hizi kukuta kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, awali zilikuyana kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Lake Tanganyika na Simba ikafanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 na kuondoka na alama tatu.

Leo ni mchezo mwingine kabisa [CRDB Bank Federation Cup], Simba ikiwa imetoka Misri kucheza mchezo mkubwa wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wana kumbukumbu mbaya na Mashujaa FC, mwaka 2018 Mashujaa FC waliifunga Simba 3-2 uwanja wa Benjamin Mkapa na kuitupa nje ya mashindano!

Mashujaa FC wanapaswa kuchagua kufanya vizuri kwenye michuano ya CRDB Bank Federation Cup au Ligi Kuu. Bado hawana uhakika wa kubaki kwenye Ligi, wanapambana wasishuke daraja.

Nafikiri malengo makubwa ya Mashujaa ni kubaki kwenye Ligi kuliko hata ubingwa wa CRDB Bank Federation Cup kwa sababu mashindano hayo unaweza kucheza hata ukiwa Ligi ya Championship lakini ukishuka kutoka Ligi Kuu kupanda ni jambo jingine kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live