Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa, Prisons, Ihefu zimejipata baada ya AFCON

Mashujaa Mz Mashujaa, Prisons, Ihefu zimejipata baada ya AFCON

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kusimama kwa Ligi kupisha Fainali za AFCON 2023, kuna baadhi ya timu zilitumia mapumziko hayo kujipanga vizuri na baadhi ya timu zimejipata.

Tanzania Prisons imekuja tofauti, Mashujaa FC imeonesha mabadiliko, Tabora United bado ni ileile, Ihefu imeonesha mabadiliko makubwa, Singida Fountain Gate FC imedhoofika.

Azam FC bado ni ileile, Kagera Sugar imeimarika, Geita Gold ni ileile! Mabadiliko ya benchi la ufundi kwa Kagera Sugar na Tanzania Prisons yameongeza tija kwenye timu na kunaonekana kuna vitu vipya vimeongezeka.

Kagera Sugar ya Fred Felix Minziro imepanda kwenye msimamo wa Ligi hadi nafasi ya saba ikiwa na alama 22, Tanzanoa Prisons ya Ahmad Ally nayo imepanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live