Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa: Hao Simba tunao!

Mashujaa Mz Mashujaa: Hao Simba tunao!

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuvuna pointi 12 katika mechi sita za raundi ya pili, Mashujaa imechekelea matokeo hayo ikiahidi kuwa bado kazi ni ngumu ikiisubiri Simba kwa hamu, ili kulipa kisasi cha bao 1-0 ilipoumana nao Lake Tanganyika, Kigoma.

Mashujaa inayocheza Ligi Kuu msimu huu kwa mara ya kwanza, haikuwa na mwanzo mzuri hadi kufikia hatua ya wengi kuikatia tamaa wakiihusisha kushuka daraja.

Tangu kuanza kwa mzunguko wa pili imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Yanga ilipolazwa mabao 2-1, Februali 8 tangu hapo imecheza dakika 540 bila kupoteza ikiwa ni sare tatu na kushinda mitatu ikichumpa nafasi ya 13 kwa alama 21.

Timu hiyo inatarajia kuwa kibaruani tena Machi 15 ikiwavaa Simba ikisaka kulipa kisasi baada ya mechi ya awali ikiwa nyumbani Lake Tanganyika kufungwa bao 1-0.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Abdalah Mohamned 'Baresi' alisema pamoja na usajili walioufanya, lakini anafurahishwa na muunganiko ambao umeanza kuonekana akieleza kuwa kwa sasa matumaini ni makubwa.

Alisema baada ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania walioshinda bao 1-0 kwa sasa akili na nguvu zipo kwenye mechi ijayo dhidi ya Simba kuhakikisha wanaendeleza kasi yao.

"Vijana wamekubali kujitolea kuipambania timu, muunganiko unaanza kuonekana kwa sababu katika mechi zote tumnepata bao hii inaonesha straika wameamka tofauti na tulivyoanza".

"Bado ni mapema kwa sababu tulipoteza mechi nyingi raundi ya kwanza ndio maana mzunguko wa pili tunapambana kutafuta ushindi ili kuziba pengo lililotukuta mapema," alisema Baresi.

Alisema baada ya kuondoka katika msitali wa njano wanahitaji kulinda matokeo hayo kwa kila mechi kupambania matokeo mazuri ili kuweza kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live