Timu ya soka ya mashujaa ya mkoani Kigoma imetambulisha kikosi cha wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo kwa wapenzi wa soka mkoani Kigoma huku Kocha, Abdallah Barres akijigamba timu yake kufanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi mkuu ya NBC ambayo inatarajia kuanza kutumia vumbi wiki ijayo.
Akizungumzia kwenye uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Inter stars ya Burundi kocha huyo wa Mashujaa alisema kuwa usajili ambao timu hiyo imeufanya unampa nafasi ya kuona namna ambavyo timu hiyo itafanya vizuri.
Alisema kuwa wiki mbili ambazo amekaa na timu hiyo kwenye Pre Season vsiwani Zanzibar anaiona timu hiyo kwenye mafanikio msimu huu na haitakuwa timu yenye historia ya kupanda daraja na kushuka kwa msimu mmoja.