Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa FC yamnasa rasmi Karihe wa Mtibwa

Karihe Pic Data Seif Abdallah Karihe

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutajwa kutaka kumsajili Denis Nkane wa Yanga, Klabu ya Mashujaa FC imekamilisha usajili wa straika wa Mtibwa Sugar, Seif Abdallah Karihe, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Karihe amesajiliwa kuziba pengo la Adam Adam ambaye ametimkia Azam FC na kutangazwa rasmi kama ni mchezaji wa timu hiyo kwa msimu ujao.

Mtoa taarifa amesema usajili wa Karihe haukuwa na tatizo sana kwa sababu tayari klabu yake imeshuka daraja, lakini yeye mwenyewe akiwa katika ubora wa hali ya juu, hivyo pande zote mbili zilikuwa zinahitajiana.

"Tayari Karihe amepewa mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika 2025, kilichobakia ni kutangazwa rasmi tu, lakini haiwezekani kufanya hivyo mpaka tutakapomaliza usajili wote ndiyo tutaanza kutupia mchezaji mmoja mmoja kwenye ukurasa wa mitandao yetu ya kijamii," alisema mtoa habari wetu.

Siku chache zilizopita, mtoa taarifa hiyo alilipenyezea taarifa gazeti hili kuwa klabu hiyo iko kwenye mazungumzo na winga wa Yanga, Nkane ambaye amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi hicho.

Alisema Nkane anamaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga kwani alijiunga 2022 akitokea Biashara United ya Mara.

"Nilikwambia kuhusu Nkane, huyu dili halijakamilika kwa sababu kuna klabu zingine zinamhitaji, unajua mchezaji ambaye anatakiwa sana, hawezi kusaini haraka, anaangalia wapi wataweka pesa nyingi, hilo ndilo linatukwamisha," alisema mtoa taarifa huyo.

Nkane anatajwa kwenda kuchukua nafasi ya Omari Abdallah Omari, ambaye taarifa zinadai amesajiliwa na Klabu ya Simba.

Mtoa taarifa huyo alisema maandalizi yote ya msimu ujao yanaelekea kukamilika, ikiwamo suala la usajili na Ijumaa ijayo, wanatarajia kukwea boti kwenda Zanzibar kwa ajili ya kupiga kambi, tayari kwa kujiandaa na Ligi Kuu msimu wa 2024/25.

"Tarehe 28 mwezi huu tunategemea kuanza maandalizi ya msimu ujao 'pre-season' mjini Zanzibar, tukiwa na wachezaji wetu wote na ndiyo utakuwa wakati wa kuanza kuwatangaza," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live