Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa FC waahidiwa mkwanja mmono kila bao vs Mbeya City

Mashujaa Mbeya City Er Mashujaa FC waahidiwa mkwanja mmono kila bao vs Mbeya City

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesho Juni 24 pale jijini Mbeya kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya Wenyeji Mbeya City dhidi ya Mashujaa Fc kutokea Kigoma kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Playoff ambapo utapigwa katika dimba la Sokoine.

Klabu ya Mashujaa Fc wao wameahidiwa hela za kitanzania Shilingi laki sita 600,000 kwa kila goli huku wenyeji wao Mbeya City mashabiki wameahidiwa kuingia bure kushuhudia mchezo huo.

Taarifa zinaeleza kuwa mashabiki zaidi ya 200 kusafiri kutoka Kigoma kuelekea mbeya kushuhudia mechi hiyo huku wengeni kutokea Dar es salaam na mikoa mingine yote ni kuisapoti timu yao ya Mashujaa ikiwa katika ardhi ya Ugenini.

Mashujaa Fc walifanikiwa kushinda magoli matatu kwa moja katika dimba la Lake Tanganyika uwanja ulifurika kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: