Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa FC: Simba SC wameponyoka mtegoni

Simba Sports Clubb Mashujaa FC: Simba SC wameponyoka mtegoni

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Mashujaa FC wamesikitishwa kuona mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC iliyotarajiwa kuchezwa Oktoba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika imeondolewa katika ratiba na kudai waliihitaji sana kwa ajili ya kujitangaza.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Nahodha wa timu hiyo, Said Makapu amesema walikuwa wamejiandaa vyema na mechi hiyo ambayo walifahamu ingeshuhudiwa na mashabiki wengi huku wao wakitaka kuonyesha ubora wao.

Makapu, ambaye aliwahi kuichezea Young Africans, amesema kila mchezaji alikuwa anajua ndiyo siku yao ya kujiweka sokoni, lakini baada ya kuahirishwa wamenyong’onyea ingawa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuivaa Coastal Union.

“Tunajua Simba SC ni timu kubwa, tunawaheshimu lakini tulikuwa tayari kuwavaa, kila mtu alihitaji kuonyesha uwezo wake, sisi kama wachezaji tulikuwa tunaitamani sana hiyo mechi kwa sababu kila mmoja alitaka kuonyesha ana uwezo kiasi gani ili kumrahisishia kwenye soko.” Amesema Makapu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live