Wachezaji watano kati ya sita wa Yanga SC waliokosekana katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya NBC tuliocheza ugenini kati dhidi ya Namungo FC akiwemo Pacome Zouzoua na Djigui Diarra, wamerejea kikosini na kufanya mazoezi leo Jumapili.
Wengine ambao walikosekana lakini wamerejea mazoezini leo ni Joseph Guede, Kennedy Musonda na Lomalisa Mutambala, tayari kwa kujiandaa na mchezo wa kesho Jumatatu dhidi ya Ihefu tutakaocheza Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:00 jioni.
Wachezaji hao walikosekana kwa sababu tofauti, huku Khalid Aucho ndiye pekee atakosekana kesho kutokana na hivi karibuni kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti.
Kurejea kwa wachezaji hao, kunatoa wigo mpana kwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kuiandaa timu na kupanga kikosi cha maangamizi hapo kesho.