Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashine tatu zarudi Yanga

Mashine Pic Data Mashine tatu zarudi Yanga

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author KIKOSI cha Yanga kinachoisaka rekodi iliyowekwa na Azam ya kucheza mechi nyingi za Ligi Kuu Bara, kinatarajiwa kupaa kesho mchana kwenda Mbeya kwa ajili ya mechi yao ya 19 msimu huu, huku jeshi hilo likiongezewa mzuka baada ya nyota wake watatu waliokuwa majeruhi kurejea.

Nyota hao wawili wa eneo la ushambuliaji Michael Sarpong na Yacouba Songne pamoja na beki wa kati mpya, Dickson Job waliokuwa majeruhi wamepona na wanatarajiwa kuwepo kwenye msafara huo wa Mbeya, huku Saido Ntibazonkiza akichomolewa na Kocha Mkuu Cedric Kaze.

Kabla ya safari hiyo, Yanga ilikuwa ikikabiliwa na majeruhi watano katika kikosi chao waliotishia ufanisi wa ushindi katika timu yao na sasa taarifa rasmi kocha Kaze presha imeshuka baada ya kurejea kwa wachezaji wake hao .

Akizungumza na Mwanaspoti mapema jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuna maendeleo mazuri kwa idadi ya wachezaji waliokuwa majeruhi baada ya washambuliaji Sarpong na Yacouba kurejea kundini. Nyota hao kila mmoja amefunga mabao manne katika Ligi Kuu Bara kabla ya kusimama Januari 3, huku timu yao ikiwa kileleni na alama za 44 baada ya mechi 18.

Hafidh alisema mbali na washambuliaji hao kurejea uwanjani pia beki wao mpya Dickson Job aliyekuwa ameumia mazoezi ya siku ya pili alipojiunga kwa mara ya kwanza na timu hiyo naye amerejea na kwamba kikosi chao kitawafuata Mbeya City wakiwa kamili gado.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz