Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashine hizi ndizo zinatua Yanga dirisha dogo

Kennedy Musonda.jpeg Kennedy Musonda

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mabosi wa Yanga wakimalizana na mshambuliaji wa Power Dynamo ya Zambia, Kennedy Musonda uongozi wa timu hiyo upo katika hatua za mwisho kumpata mmoja kati ya mabeki wakubwa Afrika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga tayari imeshamalizana na Mzambia, Musonda aliyefunga mabao 11 katika mechi 17 za Ligi Kuu ya Zambia msimu huu, kwa sasa anasubiriwa kutangazwa na mabosi wa timu hiyo.

Championi Jumatano linafahamu kuwa, Musonda ambaye alikuwa akiwindwa na Simba na TP Mazembe, wikiendi iliyopita alikuwepo nchini kumalizana na mabosi wa Yanga kabla ya kurejea Zambia kuweka vitu vyake sawa kabla ya kurejea nchini hapa.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa wanatarajia kufunga usajili wa dirisha dogo na wachezaji wawili wa kimataifa ambao hakutaka kuweza wazi majina na sehemu wanayotokea licha ya Championi kufahamu mmoja kati ya wachezaji hao akiwa ni Musonda.

“Tayari katika usajili wa dirisha dogo tumeshamtangaza kiungo Mudathir Yahya ambaye kila mmoja ameona uwezo wake katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, huo siyo mwisho wetu kwa sababu tunatarajia kukamilisha usajili wetu wa dirisha dogo na nyota wawili kutoka nje ya nchi.

“Tutasajili katika idara ya ushambuliaji na nafasi ya beki wa kati. Wachezaji ambao tunawaleta ni wakimataifa na tunawatoa kwenye mashindano yaani wanakuja kuingia kwenye mfumo wa timu kutokana na kipindi hiki cha dirisha dogo kinavyokuwa, beki tunayemleta ni beki wa kazi kweli, hao washambuliaji wetu wajipange vizuri,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live