Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashine Mpya Yaahidi Mabao Yanga

Mtambo Yanga Mashine Mpya Yaahidi Mabao Yanga

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JEMBE jipya la Yanga, Chico Ushindi amefunguka kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga ambazo zitawafanya mastraika wa timu hiyo wakiongozwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo kufunga mabao ya kutosha.

Ushindi ambaye anamudu kucheza winga zote ni usajili mpya kwa Yanga ambaye amesajiliwa kwa mkopo akitokea katika Klabu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo.

Ushindi aliweka wazi kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji wa timu hiyo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga katika michezo mbalimbali ambayo wanashiriki msimu huu.

“Yanga tayari nimeshaona jinsi ambavyo wanacheza, ni timu ambayo inatumia sana wachezaji wa pembeni katika kutengeneza nafasi za kufunga. Mimi pia nacheza huko hivyo naona nafasi ya kutengeneza zaidi nafasi za kufunga kwa washambuliaji wa kati.

“Kusajiliwa na kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara ni jambo jingine, hivyo ngoja tuone itakuwaje lakini nahitaji kucheza ili kuweza kuisaidia Yanga kufanya vizuri pamoja na kubeba ubingwa wa ligi kuu,” alisema winga huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live