Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabikiwa Yanga wapewe maua yao

Mashabiki Wa Yangaa Mashabikiwa Yanga wapewe maua yao

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kuna mashabiki wanaukumbuka Uwanja wa Benjamin Mkapa basi ni mashabiki wa Yanga, timu yao iko kwenye moto na wana morali kubwa ya kuja kwenye mechi zao lakini uwanja haukubaliani na idadi yao.

Yanga imekuwa ikishinda vizuri ndani ya Azam Complex pengine kuliko hata Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini bado kuna mashabiki wengi wanalazimika kuukosa mchezo huo kutokana na nafasi ndogo, kwani unaingiza watu wasiozidi 10,000, wakati Kwa Mkapa unabeba watazamaji 60,000.

Yanga mbali na kaundika rekodi ya kutinga makundi kwa mara ya pili ikiwa ni baada ya miaka 25 iliyopita, imeandika historia pia ya kuitoa kwa mara ya kwanza timu kutoka Sudan.

Pia, kuishinda Al Merrikh ambayo kwenye mechi nne za awali walizowahi kukutana ilikuwa haijashinda zaidi ya sare mbili za nyumbani na kupoteza ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: