Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabikiwa Simba wamekosa matumaini na timu yao - Mchambuzi

Mashabiki Simba Kwa Mkapa.jpeg Mashabikiwa Simba wamekosa matumaini na timu yao - Mchambuzi

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka EA Radio, Stephen Abissay amesema kuwa mashabikiwa Klabu ya Simba ni kama wamekosa matumaini na timu yao iwapo itaweza kufanya vizuri kwenye michauno ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kauli hiyo ya Abissay inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Simba kufanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuiondoa Power Dynamos huku mashabiki wakidai kuwa timu yao haichezo soka la kuvutia.

Ikumbukwe kuwa ndani ya misimu mitano, Simba imekuwa ikitinga hatua ya makundi ya michuano ya CAF lakini inaishia hatua ya robo fainali tu.

"Kinachowaudhi (mashabiki wa Simba) ni kwamba wanakosa matumaini ya kuona wanaweza kufika mbali kwa sababu hawaoni timu yao ikiwa inashawishi kufika mbali na hiyo ndio story kubwa zaidi," amesema Stephen Abissay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live