Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wavamia uwanja Ireland

Grsfcgf Mashabiki wavamia uwanja Ireland

Sun, 14 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa timu za Ligi Kuu Ireland Dundalk na Drogheda United, walivamia uwanja na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe mara tu baada ya mchezo uliozikutanisha timu zao uliopigwa jana, kwenye uwanja wa Orel Park.

Video ilionyesha mashabiki wakivamia uwanja na kuanza kupigana ngumi, pia shabiki mwengine alionekana akimpiga shabiki wa timu pinzani mateke wakati amelala chini.

Shabiki mmoja alionekana akitumia bendera kama silaha akielekeza kwa mashabiki wengine.

Baada ya kuibuka kwa vurugu, wachezaji walitolewa uwanjani haraka na kupelekwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa usalama zaidi.

Walinzi wa uwanjani walizidiwa kwa sababu mashabiki walikuwa ni wengi zaidi, hivyo ikabidi polisi waingilie kati kutuliza vurugu hizo.

Timu hizo mbili zote zipo katika hatari ya kushuka daraja na katika mchezo huo Dundalk ilishinda mabao 4-2.

Chanzo: Mwanaspoti