Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki watakiwa kuwahi vyumba Tanga

Tanga Region Mashabiki watakiwa kuwahi vyumba Tanga

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa soka waliopanga kwenda kushuhudia michuano ya Ngao ya Jamii itakayofanyika jijini Tanga, kuanzia Agosti 8 hadi 13 wameshauriwa kufanya kulipia vyumba mapema kabla ya kufika ili kuepuka usumbufu.

Michuano ya Ngao ya Jamii inatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na taarifa zinasema mashabiki wengi walikosa nafasi ya kulala walipokwenda kwenye mji huo kwa ajili ya fainali ya Kombe la Azam kati ya Yanga na Azam FC.

Ushauri huo ulitolewa jana na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Hanery Mwabambe alipokuwa akizuungumzia maandal-izi ya michuano hiyo itakayoanza Jumatano ijayo.

“Maandalizi yote yapo sawa, niwahakikishie mashabiki wa soka wa Tanzania na nchi jirani kama ilivyo kawaida yetu, Tanga ni amani na amani ni Tanga, kwa hivyo tunawakaribisha mje kushuhudia michuano hii ambayo itazihusisha timu za Yanga, Simba, Azam na Singida Fountain Gate.

“Wakati wa fainali ya Azam watu wengi hawakupata vyumba, hivyo ni vyema sasa wakawa makini kwa kukata tiketi zao mapema,” alisema Mwaibambe.

Chanzo: Mwanaspoti