Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wataka aliekosa bao 2010 Kombe la Dunia ashtakiwe

Yakubu Aiyegbeni.jpeg Mashabiki wa soka wa Nigeria wameomba Yakubu ashtakiwe kwa kukosa bao la wazi

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka wa Nigeria wameomba Yakubu ashtakiwe kwa kukosa bao la wazi kwenye mechi ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.

Katika mechi ya mwisho ya Kundi B la Kombe la Dunia la FIFA 2010, Yakubu aliongoza mashambulizi ya timu ya Nigeria Super Eagles dhidi ya Korea Kusini kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban.

Super Eagles walihitaji kuishinda Korea Kusini ili wafuzu hatua ya 16 baada ya kufungwa 1-0 na Argentina na 2-1 na Ugiriki.

Yakubu Aiyegbeni alipokea pasi kutoka kwa Ayila Yussuf ambaye mpira wake uliwapita mabeki wa Korea Kusini na kutua mguuni mwake.

Kwa mshangao mkubwa, Yakubu aliutoa mpira nje badala ya kuusukumia ndani ya nyavu licha ya kuwa anatazamana na goli.

Mashabiki wa soka wa Nigeria bado hawajamsamehe mshambuliaji huyo miaka 13 baada ya kukosa bao hilo la wazi na wamekuwa wakitania anastahili kufungwa kwa kosa la kuihujumu Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live