Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wataka Fred arudi fasta

Fred Turkey Mashabiki wataka Fred arudi fasta

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Manchester United wametaka viongozi wa klabu hiyo kwenda kumsajili tena na kumrudisha kwenye kikosi kiungo Fred baada ya kuonyesha kiwango bora sana huko Fenerbahce.

Fred aliuzwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana baada ya kudumu kwenye kikosi hicho cha miamba ya Old Trafford kwa kipindi cha miaka mitano.

Ndani ya muda huo alicheza mechi 213 na kufunga mabao 14 kabla ya uhamisho wake wa Pauni 13 milioni.

Tangu atue Uturuki, Fred amekuwa moto kwelikweli, akiisaidia Fenerbahce kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Super Lig.

Fenerbahce ipo nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara na mahasimu wao Galatasaray, wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu msimu huu. Kinachovutia ni Fred bado hajaonja machungu ya kupoteza mechi kama mchezaji na ameshuhudia ushindi kwenye mechi 23 kati ya 24 alizocheza.

Mashabiki wa Man United wamevutiwa na ubora wake huko Istanbul na kutaka viongozi wao wamrudishe kwenye kikosi staa huyo wa Kibrazili.

Shabiki mmoja alisema: "Arudishwe Manchester United."

Mwingine aliongeza: "Asingeuzwa. Sijali watu wanafikiria nini, ila kiungo yetu haina injini!"

Shabiki wa tatu alisema: "Namtaka arudi United. Hatuna mikimbio kwenye kiungo."

Shabiki wa nne alisema: "Nilijua tunafanya kosa kumwacha aondoke. Yule jamaa hakuna kabisa kwenye matatizo yanayotukabili. Ana moyo wa simba na viwango anapokuwa kwenye ubora wake."

Mwingine aliongeza: "Tumeuza kiungo asiyestahili kuuzwa."

Chanzo: Mwanaspoti