Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wanamtaka Tuchel, Chelsea

Thomas Tuchel Ban Mashabiki wanamtaka Tuchel, Chelsea

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MMesikia! Mashabiki wa Chelsea wanadaiwa kuhitaji kuona kocha wao wa zamani Thomas Tuchel akirejea kweye timu hiyo, huku ripoti zikieleza kwamba Tuchel mwenyewe pia yupo tayari kufanya hivyo.

Mjerumani huyu mwenye umri wa miaka 50, ambaye kwa sasa anaifundisha Bayern Munich aliondoka Chelsea Septemba, 2022 ikiwa ni miezi kadhaa tu, tangu timu hiyo iliponunuliwa na Todd Boehly.

Kwa sasa anamalizika tu msimu na Bayern na anatarajiwa kuachana nao mwisho wa msimu huu baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano.

Inaeleza kwamba kocha huyu anaangalia uwezekano wa kurudi tena kwenye Ligi Kuu England kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Bild.

Hata hivyo ili kurudi itatakiwa kwanza kumaliza tofauti zao kati yake na bosi wa matajiri hao wa Jiji la London, Todd.

Inaeleza kwamba kulikuwa na mengi yanaendelea baina ya wawili hawa na kilichokuwa kinamkera zaidi Tuchel ni Boehly kutaka kuingilia majukumu yake.

Kuna wakati tajiri huyo alidiriki hadi kuingiza wageni kwenye vyuamba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko hukukipindi ambacho Tuchel alikuwa akiiongea na wachezaji wake jinsi watakavyoenda kupambana kwenye kipindi chapili.

Kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wa Chelsea walitoa maoni yao wakisema wanasubiri nafasi hiyo kwa hamu kuona Tuchel akirejea, wengine wakisema ikiwa atatua ataenda kuwapa matokeo wanayo yahitaji tofauti na ilivyo sasa.

Hata hivyo, Tuchel pia anahusishwa kuhitaji zaidi kuifundisha Man United ikiwa atareje England ikielezwa ameshaanza hadi mazungumzo na mabosi wa timu hiyo wanaomuangalia kama mbadala waErik ten Hag.

Vilevile Barcelona inayopitia hali mbaya ya kiuchumia pia inatamani kumsajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live