Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wamzawadia filimbi Lingard

Jesse Lingard Seoul, Korea Mashabiki wamzawadia filimbi Lingard

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard amezomewa na kupewa zawadi na mashabiki wakati anatoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Seoul, Korea Kusini alikokwenda kufanya vipimo vya afya kabla hajasaini mkataba wa kuitumikia FC Seoul inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Incheon, alilakiwa na mashabiki ambao baadhi walimzoea, huku wengine wakijaribu kumshika na miongoni mwao wakampa zawadi filimbi.

Mashabiki walimpa filimbi kwa sababu ya staili yake ya kushangilia ya kuigiza kama anapiga filimbi.

Baada ya kuwasili Lingard alifanya vipimo vya afya Jumanne iliyopita na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambayo imeshachukua mataji sita ya Ligi Kuu nchini humo na kufika fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo: Mwanaspoti