Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wampa neno Ten Hag

Mahaaaaaaaaaaaaaaa Mashabiki wampa neno Ten Hag

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Manchester United wanaamini kwamba kocha Erik ten Hag anajifukuzisha kazi mwenyewe.

Hilo limetokana baada ya kocha huyo kufanya mabadiliko mawili ya hovyo kwenye mechi za kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Liverpool uwanjani Old Trafford, jana Jumapili.

Mabao mawili ya Luis Diaz kwenye kipindi cha kwanza na lile moja la kipindi cha pili lililofungwa na Mohamed Salah, yalitokana na Liverpool kutumia vyema makossa mawili ya kiungo Casemiro na moja la bwana mdogo Kobbie Mainoo.

Ten Hag alifanya mabadiliko wakati wa mapumziko baada ya kutoa Casemiro kwenye sehemu ya kiungo na kumwingiza kinda wa miaka 20, Toby Collyer. Na wakati ubao wa matokeo ukisomeka 3-0, kwenye dakika ya 69, kocha huyo Mdachi alifanya mabadiliko mengine yaliyodaiwa na mashabiki kwamba ni ya hovyo.

Matthijs de Ligt na Alejandro Garnacho walitoka na nafasi zao kuingia Harry Maguire na Amad Diallo mtawalia.

Mashabiki wanaamini uamuzi huo haukuwa sahihi kabisa, hivyo wakatumia kurasa zao huko kwenye mitandao ya kijamii kuelezea.

Shabiki mmoja alisema: "Maguire kwa De Ligt.....safi. Garnacho kwa Amad... Ten Hag anajaribu kujifukuzisha mwenyewe kazi kwa huu upendeleo wake wa hovyo."

Shabiki wa pili alisema: "Hakika alinishtusha na yale mabadiliko."

Shabiki wa tatu aliongeza: "Unafanyaje mabadiliko ya beki wa beki wa kati wakati unatafuta mabao."

Mashabiki wa Man United walioshuhudia mchezo huo kwenye mchezo huo wa nyumbani wa Old Trafford waliona makosa kwenye mabadiliko hiyo na walizomea uamuzi wa kumtoa Garnacho.

De Ligt alishakuwa na kadi ya njano wakati anatolewa, wakati Garnacho hakuwa na mchezo mzuri kwa mujibu wa viwango vya SunSport. Hivyo, takwimu za Garnacho kwenye mchezo huo, zilionyesha kwamba kocha huyo wa Man United alikuwa sahihi kumtoa kwa maana ya kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Winga huyo wa Kiargentina alipiga pasi nne tu za mbele. Akizungumza baada ya mechi, kocha Ten Hag alikasirishwa na makocha ya wachezaji yameigharimu timu kabla ya kusema kwamba yeye si Harry Potter wakati alipokuza akizungumzia ufiti wa wachezaji wake kwenye mechi.

Ten Hag alisema: "Mimi sio Harry Potter. Lazima mtambue hilo. Kuna wachezaji watatu walianzishwa kwa mara ya kwanza kwenye msimu huu. Manuel Ugarte bado hajacheza, anahitaji kujiweka fiti.

"Baada ya hapo tutamwingiza kwenye timu. Nina hakika atasaidia. Inaweza kuchukua wiki kadhaa, au pengine mwezi, hivyo ndivyo ilivyo kwa wachezaji wengi."

Man United imepoteza mechi mbili kati ya tatu ilizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, jambo linalotia mashaka juu ya usalama wa kibarua cha kocha huyo, huku wachezaji kamari wakiamini Gareth Southgate anakwenda kuwa kocha mpya huko Old Trafford.

MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED KWENYE LIGI KUU ENGLAND 2024-25

-Septemba 14 vs Southampton (ugenini)

-Septemba 21 vs Crystal Palace (ugenini)

-Septemba 28 vs Tottenham (nyumbani)

-Oktoba 5 vs Aston Villa (ugenini)

-Oktoba 19 vs Brentford (nyumbani)

Chanzo: Mwanaspoti