Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wamchangia Ally Kamwe Milioni 1 ya faini

Ally Kamweoct 7 Mashabiki wamchangia Ally Kamwe Milioni 1 ya faini

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni masaa machache tangu Bodi ya ‘Ligi’ Tanzania kumpiga ‘faini’ ya tsh 1 milioni , Afisa Habari wa ‘Klabu’ ya Yanga, Ally Kamwe kwa kosa la kumkejeri mwamuzi Tatu Malogo, Kamwe ameweka wazi kuwa ameshachangiwa pesa hiyo na mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ally Kamwe ameweka wazi kuhusu taarifa hiyo kwa kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwa mahaba waliyomuonesha ya kumchangia kupitia ‘kampeni’ iliyoendeshwa na shabiki Jimmy Kimdoki ili kumuwezesha kulipa ‘faini’ hiyo kwa wakati na kuendelea na majukumu yake.

Aidha Kamwe ameeleza kuwa amepokea adhabu hiyo kama njia ya Mungu kutaka kuzungumza naye, kwani kupitia adhabu hiyo ameona, kusikia na kujifunza mengi, kikubwa ameuona upendo wa dhati wa mashabiki wa Yanga kwake na amewashukuru kwa kuweza kumchangia kiasi hicho cha pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live