Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki walia na kamati ya usajili Simba

Banda Sakho Data Miongoni mwa sajili mpya Simba SC, ambazo bado mashabiki hawajaona makali yao

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba wameitaka Kamati ya Usajili kujitafakari baada ya kuona wachezaji waliowasajili kushindwa kuendana na mahitaji ya klabu yao.

Hayo yamesemwa na wanachama wa Simba Tawi la Wababe wa Kimataifa lililopo Nyambwera - Tandika kwa kile walichodai kuwa kutoridhishwa na usajili uliofanyika.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Simon Mbesiga alisema kamati hiyo inabidi kulaumiwa kwa kushindwa kufanya usajili muhimu kutokana na mahitaji ya kikosi chao.

“Tumeuza wachezaji kwa bei kubwa ambao walikuwa muhimu sana kwetu lakini hilo sio tatizo. Shida inaanzia pale kwenye wale mbadala wao maana inaonekana fedha iliyotumika kuwaleta ni ndogo tofauti na ile tuliyoingiza,” alisema.

Msemaji wa tawi hilo Omary Abdallah alisema kuwa katika miaka minne ya mwekezaji wao Mohamed Dewji ‘Mo’ kuna mambo wamefaulu lakini mengine wameanguka.

“Kwenye ubingwa hapa Bara tumefanikiwa lakini kwenye michezo ya kimataifa usajili umekuwa unatuangusha, ni wakati kwa Kamati ya Usajili kufanyia marekebisho,” alisema.

Mjumbe wa tawi hilo, Keto Mohamed alisema kuwa kamati hiyo inapaswa kulaumiwa kwa sababu haiwezekani kuchukua benchi la ufundi ambalo halina sifa zinazotakiwa.

“Wenzetu walishiriki hii michuano lakini hatukusikia ikiwatokea iweje kwetu tu? hii ni kuonyesha kuwa viongozi wetu hawako makini kabisa kwa sababu huwezi kumwajiri mtu ambaye hana sifa zinazotakiwa,” amesema.

Naye Ababuu Jongo ambaye ni mjumbe kwenye tawi alisema sio muda wa kulaumiana, bali wanatakiwa kutulia ili kuweka mikakati itakayowavusha mbeleni.

“Bado tuko kwenye michuano ya kimataifa kwa maana ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ni muda wa kukaa chini kwa viongozi wetu na kurekebisha kasoro zilizojitokeza,” amesema.

Tawi hilo lilianzishwa mwaka 2019 lina wanachama 51 na viongozi ni mwenyekiti Simon Mbesiga, msaidizi wake Frida Peter, katibu mkuu Shaban Mndolwa, msaidizi wake ni Daniel Mwaikenda, mtunza fedha Bushiri Ally na msemaji ni Omary Abdallah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live