Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki walia na benchi la Ufundi Azam

LWANDAMINA1?fit=700%2C400&ssl=1 Kocha Mkuu wa Azam George Lwandamina

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Juzi Jumamosi kupokea kichapo cha mabao 1-0 dhidi ya Wanajangwani katika dimba la Mkapa Jijini Dae es Salaam.

Mashabiki na Wapenzi wa wana lamba lamba, Azam FC, wameulalamikia uongozi wa klabu kwa kusema kuwa benchi la ufundi limeshindwa kazi yake hivyo linapaswa kuondolewa na kuja mwalimu atakaekidhi matakwa ya Klabu.

Mashabiki wanaosafiri na timu hiyo katika michezo yake maeneo mbali mbali wamedai kuwa katika michezo yote waliyocheza timu haionekani kuimarika bali kila siku ubora unazidi kupungua.

"Tajiri atoe huyu kocha na wasaidizi wake kazi imewashinda, kwa mechi hii tu Yanga wana watu ambao sisi hatuna lakini kiuhalisia na sisi tuna watu ambao wakipata mwalimu viwango vyao ni hatari"

"Aucho katutawala kila mahali, imefikia mpaka mtu kama Nado anarudi kuja kutafuta mpira kwa kuwa hapelekewi mipira na mwalimu hana mbinu mbadala, takjiri kama anataka tifike mbali aondoe huyu kocha" amelalama shabiki wa Azam

wakati shabiki mwingine amesema "Timu ina kila kitu ambacho hata Simba na Yanga hawana, ila wao wanafanya vyema kulinganisha na sisi, sasa tumuondoe huyu mapema kabla hajatupeleka pabaya maana sisi sio washindani tena"

Azam ilitolewa kwenye Kombe la Shirikisho na katika Ligi imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Namungo, lakini uongozi bado haujazungumza lolote juu ya Kocha wa kikosi hicho George Lwandamina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live