Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wajeruhiwa uwanjani

Mashabiki Wajeruhiwa Uwanjani Mashabiki wajeruhiwa uwanjani

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki 11 wa ‘soka’ wamejeruhiwa baada ya fataki kurushwa wakati wa ‘mechi’ ya Bundesliga kati ya ‘klabu’ Augsburg na ‘klabu’ Hoffenheim nchini Ujerumani, siku ya jana.

Kwa mujibu wa Polisi, fataki hiyo ilirushwa kutokea upande wa uwanja wa WWK Arena, kelele kubwa ilisikika uwanjani hapo huku watu kadhaa wakijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.

Kutokana na tukio hilo mchezo ulisimamishwa wakati wa huduma za dharura zikitolewa na baadaye mchezo uliendelea na kuishia kwa matokeo ya 1-1.Polisi wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na washukiwa wawili tayari wamekamatwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live