Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki waivamia Simba mazoezini

Simba+pic Mashabiki waivamia Simba mazoezini

Mon, 15 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author BAADA ya Afisa Habari wa Simba, Haji Manara kutangaza kwamba katika mchezo wao wa kesho kutwa  (Jumanne) hawatoruhusiwa kuingiza mashabiki, basi katika mazoezi ya leo Machi 14, 2021 jioni mashabiki wa tawi la Simba mpira pesa waliibuka katika uwanja wa mazoezi, Mo Simba Arena.

Manara jana Jumamosi akizungumza na waandishi wa habari alisema wamepokea taarifa kutoka Shirikisho la soka Afrika (CAF) likiwataka kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani kutokana na janga la ugonjwa wa COVID 19.

Mashabiki hao walifika uwanjani na gari aina ya Coaster na walianza kushangilia muda wote wakati Simba wakifanya mazoezi.

Staili yao ya kushangilia ilikuwa ni kupiga ngoma huku wakiimba nyimbo mbalimbali za furaha pamoja na kutaja majina ya wachezaji.

Simba itakuwa na mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Al Merikkh mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni.

Simba wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 7, As Vita pointi 4, Al Ahly pointi 4 huku Al Merikkh wakiwa na pointi 1.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz